Umoja wa Mataifa waonywa juu ya kuongezeka vifo Somalia
20 Oktoba 2023Matangazo
Catriona Laing, mwanadiplomasia wa Uingereza aliyechukua wadhifa huo mapema mwaka huu, aliliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa siku ya Alkhamis (Oktoba 19) kuwa hali hiyo imesababishwa na uasi wa wanamgambo wa kundi la al-Shabaab na mapigano katika eneo lililojitenga la Somaliland.
Laing alisema tangu kuanza kwa mwaka huu, raia wapatao 1,289 wameuawa.
Soma zaidi: Marekani yatangaza zawadi nono kwa taarifa juu ya Al-Shabab
Al-Shabaab imekuwa ikiendesha uasi dhidi ya serikali ya Somalia kwa zaidi ya miaka 15 sasa.
Rais Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia aliyeingia madarakani mwezi Mei 2022, ameapa kupambana vilivyo na kundi hilo la kigaidi.