Umoja wa Mataifa wasema idadi ya vifo yaongezeka Haiti
20 Aprili 2024Ripoti ya Ofisi ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Haiti, BINUH imeelezea hali hiyo ya Haiti hapo jana.
Ripoti hiyo inasema kuwa takribani watu 590 waliuawa wakati wa operesheni za polisi. Wengi wa watu hao hawakuhusika na vurugu za magenge, baadhi walikuwa walemavu, huku wengine 141 wakiuawa na makundi yenye silaha.
Soma pia:Mamia ya mashirika yaiomba Marekani kutowarejesha raia wa Haiti wanaokimbia machafuko
Ghasia nyingi zilitokea katika mji mkuu wa nchi hiyo, Port-au-Prince, huku takriban watu 438 wakitekwa nyara katika eneo la Artibonite.
Wafuasi wa magenge waliwabaka wanawake na wasichana
Ripoti hiyo imeongeza kuwa wafuasi wa magenge hayo walifanya ubakaji dhidi ya wanawake na wasichana katika maeneo ya wapinzani wao pamoja na magerezani na kambi za wakimbizi.