Umoja wa Mataifa wasikitishwa na msaada wa Yemen
17 Machi 2022Umoja wa Mataifa umeelezea kusikitishwa kwake baada ya mkutano wa kuchangisha fedha kwa ajili ya Yemen kukusanya chini ya theluthi moja ya dola bilioni 4.27 ulizosema unahitaji ili kuzuia janga la kibinaadamu kwenye nchi hiyo iliyoharibiwa kwa vita.
Mkuu wa masuala ya kiutu wa Umoja wa Mataifa, Martin Griffiths amesema walisikia wafadhili 36 wakiahidi karibu dola bilioni 1.3 kwa ajili ya kukabiliana na mzozo wa kiutu Yemen.
Amesema hilo ni jambo la kusikitisha kwamba wameshindwa hadi sasa kukusanya ahadi kutoka kwa baadhi ya watu waliofikiri wanaweza kusikia kutoka kwao.
Griffiths amesema baadhi ya mataifa yametimiza matarajio yao.
Mkutano huo umefanyika wakati ambapo ulimwengu ukiangazia zaidi vita vya Ukraine, ambayo hadi sasa imeifunika mizozo mingine ya kiutu tangu uvamizi wa Urusi Februari 24 na kuzusha hofu kwamba mzozo wa Yemen unaweza kusahaulika.