1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

UN yatahadharisha kwamba vita vitaiteketeza Sudan yote.

25 Agosti 2023

Umoja wa Mataifa umetahadharisha kwamba vita na njaa vinatishia kuiteketeza Suda. Wakati huo mtawala wa kijeshi wa Sudan Jenerali Abdel Fattah al-Burhan ametembelea kambi za jeshi nje ya mji mkuu, Khartoum.

Sudan Trümmer nach Angriffen in Khartum
Picha: AP Photo/picture alliance

Mratibu wa masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura wa Umoja wa Mataifa Martin Griffiths, amesema vita nchini Sudan vinachochea hali ya dharura ya kibinadamu kwa kiwango kikubwa. Amesema mgogoro huu, njaa, magonjwa na watu kulazimika kuyahama makazi yao, yote hayo yanatishia kuiteketeza nchi nzima ya Sudan.

Mratibu wa masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura wa Umoja wa Mataifa Martin Griffiths.Picha: Martial Trezzini/dpa/Keystone/picture alliance

Msemaji wa ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoratibu maswala ya kibinadamu Jens Laerke ametoa taarifa hivi punde, kuhusu Sudan iliyotolewa na mratibu wa ofisi hiyo, Martin Griffiths:

Sudan:Burhan ajitokeza hadharani miezi 4 tangu vita vianze

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Jens Laerke amesema mratibu wa masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura wa Umoja wa Mataifa, Martin Griffiths pia ametahadharisha kuwa maelfu ya watoto wenye utapiamlo wanaweza kufariki iwapo hawatapata matibabu haraka. Griddiths ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kutoa ufadhili walioahidi, ili kuharakisha zoezi la kupelekwa misaada kwa watu wa Sudan.

Mtawala wa Sudan, Jenerali Abdel Fattah al-Burhan.Picha: El Tayeb Siddig/REUTERS

Ujerumani ndio mfadhili mkubwa, ikifuatiwa na Marekani, Umoja wa Ulaya na mfuko wa dharura wa Umoja wa Mataifa.

Wakati hayp yakiendelea nchini Sudan mtawala wa kijeshi wa nchi hiyo ametembelea kambi za jeshi karibu na mji mkuu wa Sudan, Khartoum ikiwa hii ndio safari yake ya kwanza nje yam ji huo mkuu tangu mzozo wa ndani ulipozuka manmo Aprili 15.

Vyanzo viwili vya serikali vimesema Jenerali Abdel Fattah al-Burhan anatarajiwa kwenda nchi jirani kwa ajili ya mazungumzo baada ya kuvitembelea vituo vya kikanda na kituo cha Port Sudan, makao makuu ya muda ya serikali.

Kiongozi wa Kikosi cha Msaada wa Haraka wa kijeshi (RSF) Mohamed Hamdan Daglo.Picha: Mahmoud Hjaj/AA/picture alliance

Mzozo kati ya jeshi linalomuunga mkono Jenerali Abdel Fattah al-Burhan na Kikosi cha Msaada wa Haraka wa kijeshi (RSF) kinachoongozwa na Mohamed Hamdan Daglo.

Takwimu za Umoja wa Mataifa zimaonesha, zaidi ya watu milioni 4.6 wamelazimika kuyakimbia makazi yao.

Vyanzo:AFP/DPA/RTRE