1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Mataifa wataka dola milioni 371.4 kwa Lebanon

8 Januari 2025

Umoja wa Mataifa umeungana na serikali ya Lebanon kutowa ombi la dola milioni 371.4 za ziada kwenye msaada wa kibinaadamu kwa ajili ya watu waliogeuzwa wakimbizi wa ndani kutokana na vita vya Israel na Hizbullah.

Mikati, Lebanon
Waziri Mkuu wa Lebanon, Najib Mikati, akiwasili eneo la kusini mwa nchi yake kukaguwa vikosi vya jeshi.Picha: Lebanese Prime Minister Office/APA/ZUMA/picture alliance

Ombi hilo ni baada ya lile la awali la dola milioni 426 la mwezi Oktoba, wakati vita vilipoanza baina ya pande hizo mbili na kusababisha maelfu ya Walebanon kukimbia makaazi yao.

Wakati huo, zilikusanywa dola milioni 250, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.

Soma zaidi: Kiongozi mpya Syria aahidi kuheshimu mamlaka ya Lebanon

Mratibu wa huduma za kibinaadamu za Umoja wa Mataifa, Imran Riza, amesema ingawa usitishaji mapigano unaleta matumaini, bado kuwa zaidi ya wakimbizi wa ndani 125,000 huku wengine kwa maelfu wakikabiliwa na ugumu wa kuanzisha upya maisha yao.

Fedha zinazoombwa sasa zinaelekezwa kuwasaidia wakimbizi milioni moja wa Kilebanon, Syria na Palestina walioathiriwa moja kwa moja na vita hivyo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW