Umoja wa Mataifa wataka Georgia kuondoa mswada kandamizi
3 Mei 2024Matangazo
Kauli yake imekuja siku moja baada ya bunge la Georgia kupitisha rasimu ya sheria hiyo kusomwa kwa mara ya pili na siku nyingine ya maandamano dhidi ya mswada huo, ambao wakosoaji wanasema ni jitihada za kuwanyamazisha wapinzani.
Katika taarifa yake Turk ameitaka serikali ya Georgia kuweka kando mara moja na kuanzisha mjadala shirikilishi, wenye kuzihusisha asasi za kiraia na vyombo vya habari.
Iwapo utapitishwa, sheria yake itahitaji asasi ya kiraia yoyote na vyombo vya habarivinayopokea zaidi ya asilimia 20 ya ufadhili wake kutoka nje ya nchi visajiliwe kama taasisi zinazopigia chapuo maslahi ya taifa la kigeni.