1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroAfrika

Umoja wa Mataifa watoa wito wa kusitisha mapigano Sudan

30 Oktoba 2025

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito wa kukomeshwa mara moja kwa ongezeko la mapigano kati ya pande zinazohasimiana nchini Sudan.

Hali ya kiutu katika mji wa El-Fasher inazidi kuwa mbaya
Wakaazi wa El-Fashir waliolazimika kuyakimbia makazi yao kutokana na mzozo unaoendeleaPicha: Muhnnad Adam/AP Photo/dpa/picture alliance

Ameyasema hayo baada ya taarifa kuwa zaidi ya watu 460 walipigwa risasi na kuuawa katika mashambulizi yaliyofanywa na wanamgambo wa Rapid Support Forces (RSF) katika hospitali ya wajawazito kwenye mji wa El Fashir.

Hofu yazidi kutanda baada ya RSF kudhibiti El fashir

Katika tamko lake, Guterres amesema ana wasiwasi mkubwa kutokana na ongezeko la mashambulizi ya kijeshi mjini hapo siku kadhaa baada ya wanamgambo wa RSF kutangaza kuwa wameudhibiti mji huo. Mzozo kati ya wanamgambo hao na jeshi uliibuka Sudan mwezi Aprili 2023.