Umoja wa Mataifa watiwa wasiwasi na kutanuka mzozo wa Sudan
27 Juni 2023Darfur, mkoa wa magharibi mwa nchi hiyo kwenye mpaka na taifa la Chad imeshuhudia machafuko ya kutisha tangu kuzuka kwa mapigano kati ya jeshi la Sudan na kikosi cha wapiganaji wenye nguvu cha RSF mnamo Aprili 15.
Naibu Mkuu wa Shirika la Kuwahudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR), Raouf Mazou, amesema wanatiwa wasiwasi kutokana na ripoti wanazopokea kutoka mkoa huo juu ya kusambaa kwa machafuko kwa kiwango cha kutisha.
Soma zaidi: Raia wa Sudan wazidi kuyakimbia mapigano
Umoja wa Mataifa wataka mapigano yakomeshwe Darfur
Amesema hali hiyo imefanya kuwa vigumu kwa watoa huduma za msaada wa kiutu kuwafikia watu wenye mahitaji.
Mazou pia amezungumzia kurejea kwa migawanyiko ya kikabila iliyougubika mkoa wa Darfur mwanzoni mwa miaka ya 2000. Wakati huo jamii za wachache zililamika kuwa zinatengwa na kunyanyaswa na serikali iliyokuwa ikiongozwa na jamii za Waarabu.