1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN yatoa dola milioni 100 kukabiliana na matukio ya dharura

31 Agosti 2024

Umoja wa Mataifa umetoa hapo jana dola milioni 100 ili kukabiliana na matukio ya dharura ya kibinadamu katika jumla ya nchi 10 katika bara la Afrika, Mashariki ya Kati, Asia na eneo la Carribean.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio GuterresPicha: ZUMA Wire/IMAGO

Joyce Msuya, Kaimu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya kibinadamu amesema mataifa hayo yanakabiliwa na ukosefu wa fedha na hivyo kupelekea mashirika ya kibinaadamu kushindwa kutoa  msaada muhimu wa kuokoa maisha ya watu.

Zaidi ya theluthi moja ya ufadhili huo mpya utatolewa kwa Yemen inayokumbwa kwa miaka 10 sasa na vita vya wenyewe kwa wenyewe pamoja na Ethiopia inayokabiliana na makundi ya uasi. Mataifa mengine yatakayopokea msaada huo ni pamoja na Myanmar, Mali, Burkina Faso, Haiti, Cameroon, Msumbiji, Malawi na Burundi.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW