1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Mataifa watoa tahadhari ya njaa Haiti na sudan

29 Mei 2023

Umoja wa Mataifa umetahadharisha juu ya kitisho kikubwa cha njaa katika ukanda wa Sahel, Sudan na Haiti.

FAO, Food and Agriculture Organisation of the United Nations, Logo
Picha: AP Graphics

Kulingana na mashirika ya chakula na kilimo ulimwenguni, FAO pamoja na Mpango wa chakula, WFP, Ukanda huo wa Sahel, Sudan na Haiti unaungana na mataifa mengine ambayo bado yanatishiwa na balaa hilo ambayo ni Burkina Faso, Mali, Afghanistan, Nigeria, Sudan Kusini na Yemen.

Ripoti ya mashirika hayo mawili imesema hali hiyo imechochewa na vizuizi vikali vilivyowekwa na wanamgambo wa jihadi, vya watu kutembea na kusafirisha bidhaa nchini Burkina Faso na Mali, mzozo wa kiusalama nchini Haiti na mapigano yaliyozuka nchini Sudan.

Ripoti hiyo aidha, imeangazia hatari iliyopo ikiwa mzozo huo wa Sudan utazidi kusambaa pamoja na hofu inayoibuliwa na uwezekano wa mvua za El Nino dhidi ya mataifa yaliyo hatarini zaidi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW