1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN imetoa wito wa dola bilioni 47 za msaada kwa mwaka 2025

4 Desemba 2024

Umoja wa Mataifa umetoa wito wa zaidi ya dola bilioni 47 kwa ajili ya misaada muhimu kwa mwaka 2025, huku ukionya kuongezeka kwa mizozo na majanga ya kimazingira kutasababisha mamilioni zaidi ya watu kuhitaji msaada.

Mratibu wa masuala ya kiutu wa Umoja wa Mataifa Tom Fletcher amewaambia waandishi wa habari mjini Geneva kwamba ulimwengu unateketea, na kukiri kwamba anausubiria mwaka wa 2025 kwa hofu kubwa. Kwenye uzinduzi wa Tathmini ya Kimataifa ya Hali ya kiutu. Fletcher amesema mizozo mikubwa huko Gaza, Sudan na Ukraine pamoja na mabadiliko ya tabianchi vinachochea zaidi hali hiyo.

Ngamia aliyekufa amelala kando ya barabara katika eneo la Somalia, Ethiopia wakati wa ukame Aprili 3, 2017Picha: Michael Gottschalk/imago/photothek
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW