1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa mataifa watoa wito wa juhudi zaidi kupambana na ukimwi

Gregoire Nijimbere3 Juni 2005

Umoja wa mataifa, umetowa wito mungine wa kuongeza juhudi za kukabiliana na ugonjwa wa ukimwi ambao umezidi kutanda. Mjini New York, makao makuu ya Umoja wa mataifa, unafanyika mkutano wa siku moja wa kuchunguza ni juhudi gani zifanyike, ili kuepusha vizazi vijavyo kuangamia kabisa.

Kofi Annan, Katibu mkuu wa UN
Kofi Annan, Katibu mkuu wa UNPicha: AP

Mkutano huo umewajumuisha wajumbe kutoka nchi 120 wanachama wa Umoja wa mataifa, miongoni hao mawaziri wa afya kiasi ya 40. Mkutano huo utakadiria hatua imeshafikiwa, kulekea malengo yaliyokuwa yamekubaliwa katika juhudi za kupambana na ugonjwa hatari wa ukimwi.

Malengo hayo yalipangwa na Umoja wa mataifa manmo mwaka wa 2000 hadi 2001 kama moja ya malengo yake katika milenia hii, ili kupunguza idadi ya wagonjwa wa ukimwi duniani hatua kwa hatua.

Kofi Annan amesema kuwa kwa hakika, Umoja wa mataifa , nchi na jumuiya ya kimataifa kwa jumla, walijaribu kadiri wawezavyo kupambana na ugonjwa huo mara tu baada ya kuripuka.

Lakini Kofi Annan hata hivyo katika hotuba yake ya ufufunguzi wa mkutano huo, alikiri kuwa juhudi zao zilifanikiwa kiasi tu.

“Jibu letu lilifanikiwa kwa upande moja. Lakini kwa upande mungine, halikuweza kukomesha ugonjwa huo.

Daima, idadi ya watu wanaoambukizwa virusi vya ukimwi ilizidi kuongezeka katika mabara yote”. Alisema Annan.

Kofi Annan aliongeza kusema kwamba ni dhahiri kuwa ukimwi umeendelea kutanda kwa kasi inayozidi juhudi za jumuiya ya kimataifa.

Na ndio sababu alisema lazima tufanye zaidi.

“Tunapaswa kufanya zaidi kuepuka kuambukiza virusi vya ukimwi.

Tunapaswa kufanya zaidi kukabiliana na ongezeko la idadi ya wanaopatwa na virusi hivyo, wengi wakiwa ni wanawake na vijana.

Tunapaswa kufanya zaidi kupunguza madhara ya maradhi ya ukimwi katika eneo la bara la Afrika, kusini mwa jangwa la Sahara na kuepuka ugonjwa huo kutanda katika maeneo mapya.

Tupambane ipasavyo na tabia za kuwatenga wagonjwa wa ukimwi. Na zaidi ya yote kabisa, tunapaswa kutafuta chanjo dhidi ya ukimwi.

Hizo ndizo changamoto kubwa tutakazokabiliana nazo.

Tukishindwa, matokeo yake yatakuwa na hatari kubwa zaidi.

Amemalizia kusema Kofi Annan.

Kwa hakika, mwaka uliopita, ulishuhudia ongezeko la idadi ya watu walioambukizwa virusi vya ukimwi pamoja pia na ile ya waliyokufa kutokana na ugonjwa huo.

Takwim kuhusu ugonjwa huo ni za kutisha. Kwani takriban watu milioni 40, tayari walikamatwa na virusi vya ukimwi. Hadi sasa asili mia 12 tu ya wale ambao walifika katika hatua ya kutumia madama ya kupooza ugonjwa huo, ndiwo tu wanaoweza kuyapata.

Kofi Annan alipongeza juhudi zinazofanywa na mashirika ya kimataifa kama lile la Umoja wa mataifa la UN Aids katika kupambana na ukimwi na lile la Fuko la kugharimu shughuli za kukabiliana na ukimwi.

Kofi Annan alipendekeza kuwa kila nchi inayopokea misaada ya kupambana na ukimwi, iunde taasi moja tu itakaoratibu shughuli zote.

Lakini pamoja na kwamba kuna nchi au mashirika yanayotumia vibaya misaada hiyo, daima shida kubwa ni uhaba wa fedha. Mpango wa Umoja wa mataifa wa kutenga bilioni 15 zaidi za dola za kimarekani ulikubaliwa, lakini baadhi ya nchi hususan Marekani inayotoa mchango mkubwa kuliko nchi nyingine yote, inatoa taratibu mno

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW