1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Mataifa waunga mkono vikwazo dhidi ya Myanmar

1 Novemba 2023

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa aliyeteuliwa kuwa mtaalamu wa haki za binaadamu, ambaye ni mpinzani wa serikali ya kijeshi ya Myanmar, ameunga mkono vikwazo vilivyowekwa hivi karibuni na Marekani, Uingereza na Canada.

Min Aung Hlaing
Mkuu wa mapinduzi ya kijeshi ya Myanmar Min Aung HlaingPicha: Sefa Karacan/AA/picture alliance

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa aliyeteuliwa kuwa mtaalamu wa haki za binaadamu, ambaye ni mpinzani wa serikali ya kijeshi ya Myanmar, ameunga mkono vikwazo vilivyowekwa hivi karibuni na Marekani, Uingereza na Canada kwa makampuni yanayotoa msaada wa kifedha kwa utawala wa kijeshi na maafisa wakuu katika serikali hiyo.

Hatua hiyo imechukuliwa baada ya kuongezeka vurugu na ukiukwaji wa haki za binaadamu katika taifa hilo la kusini mashariki mwa Asia.

Hapo jana wizara ya mambo ya nje ya Marekani, ilisema inaiwekea vikwazo kampuni ya serikali ya mafuta na gesi ambayo ndio inayochangia pakubwa pato la taifa. Maafisa watano wa serikali pia wamewekewa vikwazo. Tom Andrews mmoja wa maafisa katika ofisi ya haki za binaadamu ya Umoja wa Mataifa, amesema vikwazo hivi vinaonyesha kwamba watu wa Myanmar hawajasahauliwa.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW