1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mataifa tajiri yaombwa kufanikisha mazungumzo ya mazingira

18 Novemba 2024

Umoja wa Mataifa amewatolea wito viongozi wa mataifa tajiri duniani wa kundi la G20 waliokusanyika nchini Brazil, kufanikisha mazungumzo ya hali ya hewa ya Umoja wa Mataifa ya COP29 yanayoendelea nchini Azerbaijan.

Azerbaijan Baku 2024 | Picha ya viongoziwalioshiriki mkutano wa kilele wa COP29
Viongozi walioshiriki mkutano wa kimataifa wa hali ya hewa, COP29 nchini Azerbaijan, ambapo Umoja wa Mataifa umetoa rai kwa mataifa tajiri kutimiza ahadi za kukabiliana na athari za mabadilikoPicha: Peter Dejong/AP Photo/picture alliance

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ambaye atahudhuria mkutano wa kilele wa G20 unaoanza leo Jumatatu huko Rio de Janeiro, amesema matokeo yenye mafanikio katika COP29 bado yanaweza kufikiwa, lakini yatahitaji uongozi na maelewano kutoka kwa nchi za G20.

Mazungumzo ya COP29 mjini Baku yamekwama licha ya wiki moja ya majadiliano, huku mataifa yakishindwa kukubaliana kuhusu mkataba wa dola trilioni 1 kwa ajili ya uwekezaji wa miradi ya hali ya hewa katika mataifa yanayoendelea.

Mbali na kiwango hicho, bado kuna mivutano pia kuhusu aina ya ufadhili na nani anayepaswa kutoa fedha hizo, huku nchi za Magharibi zikiitaka China na mataifa tajiri ya Ghuba kujiunga katika orodha ya wafadhili.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW