SiasaAfghanistan
Umoja wa Mataifa wazuru Afghanistan
20 Januari 2023Matangazo
Mkutano huu sio wa kawaida kuwahi kufanywa na mjumbe wa kigeni na viongozi wa Taliban katika eneo la kusini mwa Afghanistan. Mjumbe huyo wa ngazi za juu wa Umoja wa Mataifa anayeitembelea Afghanistan katika ziara yake iliyoanza wiki hii alikutana pia na maafisa wengine mjini Kabul pamoja na wafanyakazi wa Umoja huo na mashirika ya msaada kujadili njia za kuunga mkono na kulinda haki za wanawake. Naibu gavana Maulvi Hayatullah Mubarak amemwambia mjumbe huyo wa Umoja wa Mataifa kwamba utawala wa Taliban unataka mahusiano mazuru na ulimwengu na kutowa mwito wa kuondolewa kwa vikwazo dhidi ya viongozi wa Taliban.