1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Nchi za kiarabu zasisitiza kusimamishwa mapigano Lebanon

21 Oktoba 2024

Katibu Mkuu wa Umoja wa Nchi za Kiarabu, Ahmed Aboul Gheit, amesema mjini Beirut kwamba kipaumbele kwa jumuiya hiyo ni kufikia lengo la kusimamisha mapigano mara moja nchini Lebanon.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Nchi za Kiarabu, Ahmed Aboul Gheit
Katibu Mkuu wa Umoja wa Nchi za Kiarabu, Ahmed Aboul GheitPicha: Brendan Smialowski/AFP/Getty Images

Katibu Mkuu wa Umoja wa Nchi za Kiarabu, Ahmed Aboul Gheit, amesema mjini Beirut kwamba kipaumbele kwa jumuiya hiyo ni kufikia lengo la kusimamisha mapigano mara moja nchini Lebanon, na ameitaka Israel iondoke haraka kwenye maeneo yote ya Lebanon inayoyakalia.

Alipoulizwa iwapo Hezbollah inaweza kuangamizwa, Katibu Mkuu huyo wa Jumuiya ya Waarabu alijibu kwa kusema kuwa "hakuna anayeweza kutetekeza wazo".

Wakati huo huo, mjumbe wa Marekani, Amos Hochstein, ameeleza kwamba azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lililomaliza vita vya Israel na Hezbollah mnamo mwaka 2006 linaweza kuwa msingi wa kuvimaliza vita vinavyoendelea sasa lakini litahitaji hatua thabiti na sio kauli tupu kutoka kwa pande zinazopigana.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW