1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUbelgiji

Ulaya kujadili usitishwaji mazungumzo ya kisiasa na Israel

18 Novemba 2024

Mkuu wa sera za Nje wa Umoja wa Ulaya Joseph Borrell, amependekeza kuahirishwa kwa mazungumzo ya kisiasa na Israel kuhusu vita vyake katika Ukanda wa Gaza.

Ukraine | Vita | Josep Borrell akiwa mjinia Kyiv
Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell akizungumza wakati wa mahojiano na shirika la habari la AFP mjini Kyiv, 11/11/2024Picha: Genya Savilov/AFP/Getty Images

Borrell amependekeza hayo leo kuelekea mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya wanaokutana mjini Brussels Ubelgiji.

Borrell amesema hatua hiyo inajiri baada ya Israel kupuuza kwa mwaka mzima, miito ya kuitaka kuheshimu sheria ya kimataifa katika vita vyake Gaza.

Israel ilianza mashambulizi dhidi ya wanamgambo wa Hamas baada ya kundi hilo kushambulia Israel mnamo Oktoba 7 mwaka uliopita na kusababisha vifo vya watu 1,200 na kuwateka mamia kadhaa.

Mnamo siku ya Jumapili, jeshi la Israel lilifanya wimbi la mashambulizi katika mji mkuu wa Lebanon Beirut.

Vilevile katika Ukanda wa Gaza, makumi kadhaa ya watu Wapalestina wameripotiwa kuuawa kufuatia mashambulizi ya Israel.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW