1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Ulaya kuchukua jukumu huko Gaza

3 Februari 2008

Mratibu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya, Javier Solana, amesema umoja huo uko tayari kuwa na jukumu katika Ukanda wa Gaza ikiwa suluhisho la kisiasa litapatikana.

Solana ameyasema hayo akiwa katika ziara ya siku mbili nchini Misri baada ya kukutana na waziri wa mashauri ya kigeni wa nchi hiyo, Abu al Gheit.

Viongozi hao wamejadili kuhusu mzozo wa kisiasa nchini Lebanon na mkutano wa jumuiya nchi za kiarabu utakaofanyika hivi karibuni nchini Malta.

Hii leo Misri imeufunga mpaka wake na Gaza uliokikukwa siku 11 zilizopita wakati wanamgambo wa kundi la Hamas walipotengeneza njia na kuwaruhusu wapalestina wakimbie kutoka Ukanda wa Gaza kuingia Misri.

Maafisa wa usalama wa Misri wametumia nyaya za sing´eng´e na vizuizi vya chuma kukarabati sehemu ya mpaka iliyobomolewa.

Duru zinasema mamia ya maafisa wa usalama wa Misri wamepelekwa kushika doria kwenye mpaka kati ya Gaza na Misri.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW