1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Ulaya kufungua njia ya misaada kwa ajili ya Gaza

8 Machi 2024

Njia ya misaada ya kiutu inayoruhusu misaada kuwasilishwa Gaza kutoka Cyprus inatarajiwa kufunguliwa mwishoni mwa wiki hii.

Malori yaliyobeba misaada ya kibinadamu yanaingia katika Ukanda wa Gaza kupitia Rafah
Malori yaliyobeba misaada ya kibinadamu yakiingia katika Ukanda wa Gaza kupitia RafahPicha: Said Khatib/AFP

Haya yamesemwa leo na Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen. Von der Leyen amesema wataifungua njia hiyo Jumamosi au Jumapili. Zaidi alisema "Na tunajua ugumu uliopo katika mipaka ya ardhini ya Gaza, iwe kivuko cha Rafah au kupitia njia ya barabara ya Jordan. Na ndio maana leo Jamhuri ya Cyprus, Halmashauri Kuu ya UIaya, Falme za Kiarabu na Marekani na bila shaka zikiungwa mkono na washirika wengine muhimu, wametangaza nia ya kufungua njia ya majini ya kuwasilisha misaada zaidi ya kiutu inayohitajika mno kwa njia ya bahari." Hayo yakiarifiwaMkuu wa Shirika la haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa Volker Turk amesema, makaazi ya Waisraeli katika maeneo yaliyokaliwa na Wapalestina yameongezeka pakubwa. Turk ameongeza kwamba hatua hiyo inaleta hatari ya kuondoa uwezekano wowote wa kuwepo kwa taifa la Palestina. Mwezi uliopita, Marekani ilisema makaazi hayo yanakiuka sheria za kimataifa baada ya Israel kutangaza mipango mipya ya ujenzi wa nyumba katika Ukingo wa Magharibi.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW