1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa ulaya kuikopesha Ukraine Euro bilioni 35

22 Oktoba 2024

Bunge la Ulaya limepiga kura ya kuipatia Ukraine mkopo wa Euro bilioni 35, pesa hizo ni sehemu ya faida ya mali za urusi ambazo zinashikiliwa na mataifa hayo ya Umoja wa Ulaya.

Bunge la EU | Mjadala wa Mashariki ya Kati
Mjadala wa Mashariki ya Kati ndani ya moja kati ya vikao vya Bunge la Umoja wa UlayaPicha: FREDERICK FLORIN/AFP

Serikali ya Ukraine inahitaji msaada wa kifedha ili kuimarisha uchumi wake, kuandaa jeshi lake na kuhakikisha kuwa gridi yake ya umeme inafanya kazi hasa msimu huu wa baridi wakati vikosi vya Urusivikizidisha mashambulizi katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo. Mkopo huo wa Umoja wa Ulaya ambao uliidhinishwa na wabunge wengi ni sehemu ya mpango mkubwa wa dola bilioni 50 uliokubaliwa na mataifa yenye nguvu ya G7 mwezi Juni kwa Ukraine. Mkopo huo wa hivi punde unakamilisha idadi ya takriban euro bilioni 120 za msaada ambazo nchi nwananchama za Umoja wa Ulaya zimetoa kwa Ukraine tangu uvamizi wa Urusi nchini humo mwaka 2022.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW