1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiMisri

Umoja wa Ulaya kuipa Misri ufadhili wa euro bilioni 7.4

17 Machi 2024

Viongozi wa nchi za Ulaya wameidhinisha siku ya Jumapili ufadhili wa kifurushi cha mabilioni ya euro kwa Misri na kuboreshwa kwa mahusiano na taifa hilo.

Rais wa Halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen akisalimiana na  rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi
Rais wa Halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen akisalimiana na rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi baada ya EU kuidhinisha ufadhili wa dola bilioni 7.4 kwa taifa hiloPicha: Dati Bendo/EU Commission/dpa/picture alliance

Hatua hiyo ni sehemu ya mpango wa kushinikiza kuzuia mtiririko wa wahamiaji wanaopitia katika Bahari ya Mediterania kuingia ulaya. Umoja wa Ulaya umetangaza hivi punde kuidhinisha msaada wa euro bilioni 7.4 kwa Misri.

Kwa muda mrefu, serikali za nchi za Magharibi zimekuwa na wasiwasi kuhusu hali ya sintofahamu katika nchi ya Misri yenye watu milioni 106, ambayo imekuwa ikikabiliwa na  matatizo makubwa ya kiuchumi  na hivyo kupelekea idadi inayoongezeka ya watu kuihama nchi hiyo.

Mpango huo ambao umekosolewa na mashirika ya kutetea haki za binaadamu, unalenga kuimarisha ushirikiano katika sekta za nishati mbadala, biashara na usalama. Fedha hizo zitatolewa kama misaada, mikopo na ufadhili mwingine katika kipindi cha miaka mitatu ijayo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW