Umoja wa Ulaya kuipatia Lebanon msaada wa dola bilioni moja
2 Mei 2024Matangazo
Von der Leyen ambaye ameambatana na Rais wa kisiwa cha Cyprus Nikos Christodoulides ametangaza kuwa Umoja wa Ulaya utaipatia Lebanon msaada wa euro bilioni 1 ili kusaidia kukuza uchumi wa taifa hilo.
Soma pia:EU kuliwekea vikwazo jeshi la Walinzi wa Mapinduzi wa Iran
Mkuu wa majeshi wa Lebanon, Joseph Aoun na waziri wa mambo ya kigeni Abdallah Bou Habib ni miongoni mwa waliohudhuria mkutano huo.
Lebanon, yenye zaidi ya wakimbizi 800,000 wa Syria wanaoishi katika umasikini mkubwa, imekuwa ikikabiliwa na mgogorowa uchumi tangu mwaka 2019.