1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Ulaya kuitambuwa Kosovo

10 Desemba 2007

BERLIN

Umoja wa Ulaya utaitambuwa kwa haraka Kosovo iwapo itajitenga na Serbia.

Wolfgang Tschinger mwakilishi wa Umoja wa Ulaya katika mazungumzo yaliomalizika hivi karibuni juu ya Kosovo amesema kwenye mahojiano ya radio kwamba uamuzi juu ya hilo yumkini ukafikiwa hivi karibuni.

Lakini amesema kwamba Umoja wa Ulaya utasisitiza kwamba Kosovo ilio huru inaheshimu sheria zinazolinda haki za makabila ya watu wachache na kuidhinisha katiba mpya ambayo tayari imerasimiwa.

Wakati huo huo msemaji wa timu ya usulihishi ya Kosovo amesema wataanza mazumgumzo mara moja na mataifa ya magharibi yanayoiunga mkono kuelekea kujitangazia uhuru kwa jimbo hilo ambapo amesema suala sasa sio tena iwapo bali lini.

Mawaziri wa Umoja wa Ulaya wamewasili Brussels Ubelgiji leo hii kujaidili mustakbali wa jimbo hio la Serbia lililojitenga wakati Urusi ikionya juu ya matokeo mabaya ya kujitangazia uhuru kwa jimbo hilo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW