1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Ulaya kulazimika kuiongezea msaada Ukraine

16 Februari 2024

Umoja wa Ulaya utalazimika kuongeza maradufu msaada wake wa kijeshi kwa Ukraine ili kuziba pengo lililoachwa na Marekani, baada ya miezi kadhaa ya bunge la nchi hiyo kuzuia kutolewa kwa msaada mpya kwa Ukraine.

Mkutano wa Mawaziri wa Ulinzi wa Muungano wa Kijeshi wa NATO.
Mkutano wa Mawaziri wa Ulinzi wa Muungano wa Kijeshi wa NATO kwa ajili ya Ukraine.Picha: Ansgar Haase/dpa/picture alliance

Taasisi ya Utafiti ya Kiel inayofuatilia masuala ya msaada yenye makao yake nchini Ujerumani ilisema katika ripoti yake kuhusu hali ya msaada wa kijeshi, kifedha na kibinaadamu kwa Ukraine tangu uvamizi wa Urusi wa Februari 24, 2022, kuwa haijulikani ikiwa Marekani itatuma msaada zaidi wa kijeshi mwaka huu wa 2024.

Soma zaidi: Stoltenberg aonya dhidi ya kuigawa Marekani na Ulaya

Kulingana na takwimu zake za hadi Januari 15, 2024, Marekani ilikuwa imetuma dola bilioni 45.4 za msaada wa kijeshi kwa Ukraine kati ya Februari 2022 na Desemba 2023, ikiwa ni karibu na euro bilioni mbili kwa mwezi.

Umoja wa Ulaya na wanachama wake 27 umeahidi msaada wa kijeshi wa euro bilioni 49.7 tangu kuanza kwa vita, lakini kufikia sasa umetoa au kutenga euro bilioni 35.2 tu.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW