1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Ulaya kupeleka shehena ya silaha Ukraine

23 Machi 2023

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wapo katika maandalizi ya kuidhinisha mpango wa kupeleka Ukraine makombora milioni moja ya mizinga katika kipindi cha miezi 12 ijayo kwa ajili ya kukabiliana na uvamizi wa Urusi.

Belgien Brüssel | EU Gipfeltreffen
Picha: Olivier Matthys/AP/dpa/picture alliance

Kwa mujibu wa wanadiplomasia kadhaa wa ngazi za juu wa Umoja Ulaya, juma hili mawaziri wa mambo ya nje na ulinzi wa umoja huo waliidhinisha mpango huo wa kuharakishwa utaratibu wa ununuzi mapema, ambapo viongozi wa mataifa hayo 27 wnatarajiwa kubariki hatua hiyo katika mkutano huu wa kilele ulianza leo.

Na Ukraine inakabiliwa na uhaba wa risasi baada ya zaidi ya mwaka mmoja wa mapigano, mwezi uliopita Waziri Mkuu wa Estonia Kaja Kallas aliliwasilisha mezani wazo la Umoja wa Ulaya kuanzisha mpango wa ununuzi wa pamoja sawa na lile lililobuniwa wakati wa janga la UVIKO-19 katika kununua chanjo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW