1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Ulaya kupeleka ujumbe Aceh, Indonesia

28 Julai 2005

Brussels:

Umoja wa Ulaya, kwa mara ya kwanza kabisa, utakuwa na ujumbe wa uchunguzi barani Asia kuanzia katikati ya mwezi ujao. Wajumbe 200 wa Umoja wa Ulaya watapelekwa kusimamia utekelezaji wa mkataba wa kusimamisha vita vya wenyewe kwa wenyewe katika mkoa wa Aceh nchini Indonesia. Mkataba wa kusimamisha vita kati ya serikali ya Indonesia na Waasi wa Aceh umefikiwa kutokana na upatanishi wa Viongozi wa Finnland baada ya miaka 30 ya vita vya wenyewe kwa wenyewe. Mkataba huo utatiwa saini Agosti 15 mwaka huu. Serikali ya Jakarta baada ya vuta nikuvute sasa imekubali waasi wa Aceh waanzishe chama chao cha kisiasa. Mpaka hivi sasa ilikuwa ni marufuku kuanzisha vyama visivyokuwa vya kitaifa nchini Indonesia.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW