EU kusaidia kuandaa mkutano wa kuwarejesha watoto wa Ukraine
24 Machi 2023Matangazo
Von der Leyen amesema baada ya mkutano wa kilele wa viongozi wa Umoja wa Ulaya kwamba atashirikiana na waziri mkuu wa Poland Mateusz Morawiecki kuhamasisha msaada wa kimataifa wa kurejeshwa watoto hao.
Karibu watoto 16,200 walichukuliwa tangu kuanza kwa vita Februari mwaka uliopita, hii ikiwa ni kulingana na Kyiv.
Soma pia: UN: Urusi inawachukua kwa nguvu watoto wa Ukraine
Wiki iliyopita Mahakama ya Kimataifa ya uhalifu, ICC ilitoa waranti wa kukamatwa rais Vladimir Putin wa Urusi ikimshutumu kwa makosa ya uhalifu wa kivita ikisema alisimamia mchakato wa kuwachukua watoto hao.