1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

EU kutoa msaada wa kibinaadamu wa dola milioni 96 kwa DRC

18 Februari 2026

Umoja wa Ulaya umetangaza kuwa utatoa msaada wa kibinaadamu wa dola milioni 96 ili kuwasaidia watu walioathiriwa na mzozo unaoendelea mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

 Kamishna Mkuu wa Umoja huo anayehusika na migogoro Hadja Lahbib
Kamishna Mkuu wa Umoja huo anayehusika na migogoro Hadja Lahbib yuko ziarani mashariki mwa DRCPicha: Valentine Zeler/European Union

Hayo yameelezwa jana na Kamishna Mkuu wa Umoja huo anayehusika na migogoro Hadja Lahbib ambaye yuko ziarani katika eneo hilo huku akisisitiza kuwa raia wa mashariki mwa DRC wamenaswa katika madhila ya vita, njaa na ukimbizi na kwamba wanataabika kupata huduma za mzingi.

Pesa hizo za EU zinalenga kufadhili msaada wa chakula, huduma za afya na kuboresha usafi wa mazingira na makazi pamoja na upatikanaji wa maji  mashariki mwa Kongo , lakini pia kuwasaidia wakimbizi wa DRC waliokimbilia katika nchi za Burundi, Rwanda na Tanzania. 

Lahbib amezitaka pande zinazozozana kuyawezesha mashirika ya kibinadamu kulifikia eneo hilo akisisitiza kuwa pesa pekee haziwezi kusitisha mateso ya raia huku akitoa pia wito wa kuheshimiwa kwa sheria za kimataifa za kibinaadamu.

Umoja wa Ulaya umesema kwa sasa zaidi ya watu milioni 21 huko Kongo wanahitaji msaada wa kibinadamu huku wengine takriban milioni 28 wakiwa wameathiriwa kutokana na ukosefu wa chakula kufuatia mgogoro katika eneo hilo lenye utajiri wa rasilimali ambao umedumu kwa zaidi ya miaka 30.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW