1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiUjerumani

EU na China ziko tayari mazungumzo kuhusu ushuru wa magari

24 Juni 2024

China na Umoja wa Ulaya wako tayari kufanya mazungumzo juu ya uamuzi wa hivi karibuni wa Umoja huo wa Ulaya wa kuongeza kiasi kikubwa ushuru wa uingizwaji wa magari ya umeme kutoka China.

Moja ya magari ya umeme yanayoundwa China
Umoja wa Ulaya unailalamikia China kwa kutoa ruzuku kubwa kwa makampuni yake ya kuunda magari ya umeme. Picha: HPIC/dpa/picture alliance

Waziri wa masuala ya biashara pamoja na Waziri wa Uchumi wa Ujerumani wamesema mwishoni mwa wiki iliyopita kwamba kila upande umeonyesha utayari kuzungumzia suala hilo.

Wanasema haya wakati vyombo vya habari vya China vikisema leo kwamba Beijing inaushinikiza Umoja wa Ulaya kuachana na mipango hiyo ya kupandisha ushuru ifikapo Julai 4.

Umoja wa Ulaya ulipanga kupandisha ushuru kutoka asilimia 17.4 hadi 38.1 wa magari hayo ya umeme ya China kwa muda wa miezi minne, kuanzia Julai 4, hatua iliyochochea mzozo wa kibiashara.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW