Umoja wa Ulaya na India waingia makubaliano ya biashara huru
27 Januari 2026
Rais wa Halmashauri Kuu ya Ulaya Ursula von der Leyen pamoja na Waziri Mkuu wa India wamesema hayo mapema leo baada ya mkutano wa kilele kati ya Ulaya na India mjini New Delhi.
Amesema "Sekta ya uzalishaji itapata msukumo mkubwa kutokana na makubaliano haya ya biashara na Umoja wa Ulaya, na sekta ya huduma pia itaimarika. Mkataba wa Biashara Huria utaongeza imani ya kila mwekezaji na mfanyabiashara kuwekeza nchini India."
Bi von der Leyen amesema wameunda ukanda wa biashara huria itakayokutanisha watu bilioni 2, huku pande zote mbili zikitarajia kunufaika.
Chini ya makubaliano hayo, India inataraji kupunguza ushuru wa magari yanayoingizwa kutoka nje kutoka asilimia 110 hadi asilimia 10 na pia itaondoa ushuru wa vipuri vya magari katika kipindi cha miaka mitano hadi 10.