1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Biashara

EU na Indonesia kutia saini makubaliano ya kibiashara

22 Septemba 2025

Nchi za Umoja wa Ulaya na Indonesia zitatia saini makubaliano ya kibiashara hapo kesho Jumanne baada ya mazungumzo ya karibu muongo mmoja. Makubaliano hayo yanalenga kupunguza athari za ushuru wa Marekani.

Makao makuu ya Umoja wa Ulaya, Brussels
Brussels, UbelgijiPicha: Virginia Mayo/AP Photo/picture alliance

Makubaliano hayo, yatakayotiwa saini katika kisiwa cha mapumziko cha Bali, yataiunganisha Indonesia yenye rasilimali na jumuiya ya Ulaya yenye wanachama 27 katika uhusiano wa karibu wa kiuchumi.

Hayo yanakuwa ni makubaliano ya tatu ya kibiashara kati ya Umoja wa Ulaya umetia na nchi za kusini mashariki mwa Asia, baada ya Singapore na Vietnam.

Umoja wa Ulaya ni mshirika mkubwa wa tano wa kibiashara wa Indonesia na biashara ya pande hizi mbili ilifikia dola bilioni 30.1 mwaka jana.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW