1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Ulaya na kundi la ACP

4 Aprili 2007

Umoja wa Ulaya wenye wanachama 27 umetangaza kufungua zaidi masoko yake kwa bidhaa za nchi 77 za kundi la Afrika,Caribbean na Pacific.Afrika Kusini lakini, haitanufaika kikamilifu na mpango huo.

Umoja wa Ulaya jana uliarifu kwamba uko tayari kuondoa viwango vyote maalumu pamoja na ushuru kwa bidhaa za kilimo na za viwandani zinazoingizwa katika nchi 27 za Umoja huo.

Umoja wa Ulaya halkadhalika, unalitaka kundi la nchi 77 za Afrika-Caribbean na Pacific (ACP)zifungue pia milango ya masoko yao kwa bidhaa kutoka nchi za Umoja wa Ulaya .

Tume ya ulaya iliarifu jana kwamba inafungua masoko yake wazi kwa koloni za zamani katika mazungumzo ya kibiashara huku ikiweka kipindi cha mpito kwa mazao kama mpunga na sukari.

Mabingwa weengi kutoka kundi la nchi za ACP –nyingi kati ya hizo makoloni ya zamani ya dola za Ulaya tayari zinaingiza bidhaa zao bure bila ushuru katika soko la Umoja wa ulaya.

Mpango wa kutotoza ushuru kutoka shirika la Biashara Duniani unamalizika muda wake mwishoni mwa mwaka huu na mazungumzo ya kurefusha yamekwama hadi sasa.

Tangazo hilo la Tume ya UU linatoa sasa nafuu na kuzifanya hadi nchi 30 miongoni mwa 77 za ACP kuvuta pumzi.Kwani hivi sasa nchi hizo zalipa ushuru juu ya bidhaa kama matunda,mboga,nafaka na nyama.

Wakati huu kumekuwapo viwango maalumu vya kusafirisha bidhaa kutoka nchi hizo kwa mazao kama vile ndizi,sukari na mchele.

Afrika Kusini haitanufaika kikamilifu na mpango huu-Tume ya Ulaya imearifu na hivyo itrapaswa kulipa ushuru wa kuagiza bidhaa za aina mbali mbali za kilimo.

Tume ya Umoja wa Ulaya imepinga lawama kuwa badala ya kujadiliana mapatano ya biashara huru bila ya vikwazo na nchi za ACP-Afrika Caribbean na Pacific, Umoja wa Ulaya ungepaswa kuendelea na mapatano ya sasa ya Cotonou ambayo hayaitishi nchi changa nazo zijibishe ukarimu huo kwa kuzifungulia pia nchi za UU masoko yao.

Maafisa wa UU wanadai shirika la Biashara Duniani (WTO) linadai katika sheria zake mageuzi yafanyike katika mapatano ya cotonou na kwamba nafuu chini ya mapatano ya WTO yanamalizika mwisho wa mwaka.Maafisa wa UU wanadai zaidi kuwa mapatano ya kisasa zaidi ya biashara yanayozungumzwa sasa yatasaidia kukuza ushirikiano wa kimkoa barani Afrika na wakasema serikali za nchi za Afrika,Caribbean na Pacific zisiingie na wasi wasi mno kwa kupoteza mapatao kutokana na kuondoa vikwazo vyao vya ushuru.

Wamekanusha pia mashtaka kwamba wakulima na wanaviwanda katika nchi za ACP hawatanufaika kutokana na bidhaa za nchi za Umoja wa Ulaya katika nchi hizo changa.

Umoja wa Ulaya unajadiliana wakati huu ushirikiano wa kiuchumi na kanda 6 za Afrika,Caribbean na Pacific .Zinajumuisha ukanda wa Caribbean na Pacific,Afrika magharibi,Afrikas mashariki na kusini mwa afrika,Afrika ya kati,Kusini mwa afrika na Pacific.