1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaPoland

Poland yazuia magari ya abiria yaliyosajiliwa Urusi

17 Septemba 2023

Poland imeanza kutekeleza zuio la Umoja wa Ulaya la magari ya abiria yaliyosajiliwa kwa namba za Urusi kuingia nchini humo hii ikiwa ni miongoni mwa msururu wa vikwazo vya karibuni dhidi ya Urusi iliyoivamia Ukraine.

Eneo la mpaka kati ya Urusi na Poland kama linavoonekana baada ya kuanza kwa utekelezwaji wa hatua ya kuyazuia magari yenye usajili wa Urusi kuingia Poland, Septemba 17,2023
Eneo la mpaka kati ya Urusi na Poland kama linavoonekana baada ya kuanza kwa utekelezwaji wa hatua ya kuyazuia magari yenye usajili wa Urusi kuingia Poland, Septemba 17,2023Picha: Michal Fludra/NurPhoto/picture alliance

Waziri wa mambo ya ndani wa Poland Mariusz Kaminski amesema jana wakati akitangaza hatua hiyo kwamba gari lililosajiliwa Urusi halina haki ya kuingia Poland na utekelezaji wake ulianza usiku wa kuamkia leo.

Amesema hii ni aina yningine ya kizuizi dhidi ya Urusi na raia wake wanaohusika na vita nchini Ukraine na kutokana na ukweli kwamba taifa la Urusi linaibua kitisho wa kiusalama ulimwenguni.

Hatua hiyo inaanza kutekelezwa siku chache baada ya mataifa ya Baltiki, Lithuania, Latvia na Estonia kuzuia magari yaliyosajiliwa Urusi, wakiungana na hatua hiyo ya Umoja wa Ulaya.