Umoja wa Ulaya utayari kuwa mwangalizi, uchaguzi Tanzania
29 Juni 2020Balozi wa Umoja wa Ulaya kwa nchi za Afrika Mashariki Manfredo Fanti, amezungumza na wanahabari wa DW pamoja na Gazeti la East Afrika, ambapo mbali na mambo mengine aligusia suala la uchaguzi mkuu wa nchini Tanzania.
Tanzania ina jukumu la kuhakikisha uchaguzi huru
Balozi huyo amesema hadi sasa hakuna mazungumzo yoyote yaliyofanyikabaina ya taifa hilo la Afrika mashariki pamoja na jumuiya hizo ya kimataifa kuhusiana na suala la uchaguzi, ijapokuwa upo tayari kufanya uangalizi wa uchaguzi huo ambao utawaweka mamlakani, madiwani, wabunge na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Aidha balozi Fanti amesema taifa lina jukumu la kuhakikisha kunakuwa na uchaguzi huru, haki na amani katika kipindi chote cha uchaguzi, huku akisisitiza kuwa umoja huo hauna mamalaka ya kuangalia uchaguzi bila mamalaka husika kutoa idhini.
Itakumbukwa kuwa sehemu ya kanuni za uchaguzi zinaeleza kuwa, Tume inaweza kutuma mwaliko kwa waangalizi wa kimataifa, jambo ambalo lilitoa wasiwasi kwa vyama vya siasa hasa upinzani kwamba huenda NEC isitoe fursa hiyo kwa jumuia za kimataifa kufuatilia kwa ukaribu zoezi hilo la kidemocrasia kama ilivyofanyika kwa chaguzi zilizopita.
Uchaguzi wa Tanzania unatarajiwa kufanyika Oktoba
Katika hili Tume ya taifa ya uchaguzi nchini NEC inasema, bado haijatoa mualiko kwa jumuia za kimataifa kwa ajili ya kutazama uchaguzi kwani taratibu zinaendelea kukamilishwa na punde zitakapokamilika utaratibu utafatwa na watakaribishwa kukamilisha majukumu yao. Wakili Emanuel
Tanzania inataraji kufanya uchaguzi mkuu mnamo mwezi Octoba ambapo hadi sasa mchakato mbalimbali unaendelea kufanyika, ikiwemo vyama vya siasa kujiweka sawa katika kuweka wagombea wataowawakilisha katika uchaguzi huo watano kufanyika tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi nchini humo.