1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Ulaya waanza mkutano wa kilele na mataifa ya Ghuba

16 Oktoba 2024

Mkutano huu ni sehemu ya msukumo wa kidiplomasia wa Umoja huo kwa washirika wake wa mbali ili kuungwa mkono kimataifa katika azma yao ya kuitenga Urusi.

Umoja wa Ulaya waanza mkutano wa kilele na mataifa ya Ghuba mjini Brussels, Ubelgiji
Umoja wa Ulaya waanza mkutano wa kilele na mataifa ya Ghuba mjini Brussels, UbelgijiPicha: Michael Kappeler/AP/dpa/picture alliance

Lengo la mkutano huo ni kukutana na mataifa sita tajiri ya Kiarabu yaliyopo kwenye baraza la ushirikiano la Ghuba ili kuwa na uhusiano wa kimkakati kwa kutambua ushawishi wa nchi hizo hasa katika migogoro kama vita vya Ukraine na huko Mashariki ya Kati.

Tangu uvamizi wa Urusi nchini Ukraine,Umoja wa Ulaya wenye wanachama 27 umefanya mikutano kama hiyo na mashirika mengine ya kikanda ikiwa ni pamoja na Jumuiya ya ushirikiano wa kiuchumi na kiusalama ya nchi za Kusini Mashariki mwa Asia-ASEAN pamoja na jumuiya ya CELAC inayoyakusanya mataifa ya Carrebean na Amerika Kusini.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW