EU yahaha kukwepa ushuru wa Trump kuhusu Greenland
19 Januari 2026
Matangazo
Siku ya Jumamosi (Januari 17), Trump alitishia kuyapandishia ushuru mataifa sita ya Umoja wa Ulaya pamoja na Norway na Uingereza, hadi pale Marekani itakaporuhusiwa kukinunuwa kisiwa cha Greenland
Mataifa hayo ni Denmark, Sweden, Ufaransa, Ujerumani, Uholanzi na Finland. Mataifa makubwa ya Umoja wa Ulaya yamekiita kitisho hicho cha Trump kuwa ni ghiliba.
Viongozi wakuu wa Umoja huo wanatazamiwa kukutana mjini Brussels kwa mkutano wa dharura wa kilele hapo Alkhamis kujadili hatua za kuchukuwa.
Mojawapo ya hatua hizo ni ushuru wa euro bilioni 93 kwa bidhaa za Marekani unaoweza kuanza kazi tarehe 6 Februari baada ya kusitishwa kwa miezi sita.