1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Ulaya waikaribisha Uingereza kwa mashirikiano

2 Oktoba 2024

Rais wa Halmashauri Kuu ya Ulaya, Ursula von der Leyen, amemakaribisha Waziri Mkuu wa Uingereza, Keir Starmer, mjini Brussels hii leo na kumwalika kushirikiana kwa karibu zaidi katika nyakati hizi tete.

Waziri Mkuu wa Uingereza, Keir Starmer
Waziri Mkuu wa Uingereza, Keir Starmer.Picha: Simon Dawson/Avalon/Photoshot/picture alliance

"Tuna mengi ya kujadiliana leo, na ninatazamia sana kushirikiana nanyi na kuendelea kuimarisha uhusiano wetu." Alisema von der Leyen akimkaribisha Starmer mjini Brussels.

Von der Leyen alisema kama washirika wenye mitizamo inayofanana, ni muhimu kushirikiana kwa karibu kwa kuzingatia mitizamo yao katika masuala ya mabadiliko ya tabianchi na kuisaidia Ukraine dhidi ya uvamizi wa Urusi.

Soma zaidi: Starmer aanza mchakato wa kupunguza makali ya Brexit

Starmer yuko mjini Brussels kwa ziara yake ya kwanza katika jitihada zake za kurejesha uhusiano na Umoja wa Ulaya, ambao ulikuwa wa mashaka na serikali iliyopita ya Conservative.

Kiongozi huyo wa chama cha Labour alisema alikuwa anataka Brexit iwe ya manufaa kwa Waingereza na kutuliza mahusiano na Umoja huo ili kuimarisha uchumi na maslahi ya usalama.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW