1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Sheria na HakiAsia

EU waikosoa Mongolia kwa kutomkamata Putin

Josephat Charo
4 Septemba 2024

Umoja wa Ulaya umeikosoa Mongolia kwa kushindwa kutekeleza waranti wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC dhidi ya rais wa Urusi Vladimir Putin wakati wa ziara yake nchini humo

Mongolia | Rais Putin
Rais wa Urusi Vladimir Putin akikaribishwa kwa gwaride maalum nchini MongoliaPicha: Natalia Gubernatorova/TASS/dpa/picture alliance

Msemaji wa Umoja wa Ulaya amesema katika taarifa kwamba umoja huo unasikitika kwamba Mongolia, nchi iliyoridhia mkataba wa Roma ulioiasisi mahakama ya ICC, haikutimiza majukumu yake chini ya mkataba wa kutekeleza waranti wa kukamatwa.

Wakati haya yakiarifiwa, Umoja wa Mataifa umezikumbusha nchi zilizosaini mkataba wa Roma kwamba lazima ziheshimu mikataba ya kimataifa baada ya Putin kukwepa kukamatwa wakati wa ziara yake nchini Mongolia.

Soma pia:Putin atoa mwaliko kwa Mongolia kuhudhuria mkutano wa BRICS

Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric amesema mjini New York kwamba nchi zilizosaini mikataba ya kimataifa zina wajibu kuiheshimu na kuitekeleza, ingawa hakutaka kutoa kauli moja kwa moja kuhusu suala la Putin. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW