1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

EU yajiandaa kwa jibu la pamoja dhidi ya ushuru wa Trump

18 Januari 2026

Rais wa Baraza la Ulaya Antonio Costa, amesema Umoja wa Ulaya unatafakari jibu la pamoja baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kutangaza ushuru wa asilimia 10 kwa nchi 8 za Ulaya.

EU inajiandaa kujibu pamoja mpango wa Trump wa kuziwekea ushuru wa asilimia 10 nchi 8 za umoja huo zisizounga mkono nia yake ya kuinunua Greenland
Rais wa Baraza la Ulaya Antonio CostaPicha: EU Council/Pool/Anadolu/picture alliance

Nchi hizo ni zile zinazopinga juhudi za Trump za kuinunua Greenland. Alitangaza kuwa ushuru huo utaendelea hadi mpango wa kuinunua Greenland utakapofanikiwa na huenda ushuru huo ukatekelezwa mpaka Juni 25 kama hakuna makubaliano yatakayofikiwa.

Juhudi za kuzuia ushuru wa Trump zaendelea

Wakati huohuo, kiongozi wa walio wachache wa chama cha Democratic katika baraza la Seneti la Marekani, Chuck Schumer ameahidi kufanya juhudi za kuzuia ushuru aliotishia kuuweka Rais Trump dhidi ya washirika wa Ulaya kutokana na mzozo wa Greenland.

Katika taarifa yake iliyotolewa Jumamosi, Schumer amesema ushuru unaotangazwa na Trump wa kukurupuka umeshasababisha mfumuko mkubwa wa bei na kuuharibu uchumi wa Marekani.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW