1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Ulaya wajizatiti zaidi juu ya wahamiaji haramu

18 Oktoba 2024

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wamekubaliana kutumia uwezo wao wote ili kuharakisha zoezi la kuwarudisha wahamiaji wanaoingia kinyume cha sheria barani ulaya.

Umoja wa Ulaya wasema unajizatiti zaidi juu ya wahamiaji haramu
Umoja wa Ulaya wasema unajizatiti zaidi juu ya wahamiaji haramuPicha: Ludovic Marin/AFP/Getty Images

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wamekubaliana jana Alhamisi kutumia uwezo wao wote, ikiwa ni pamoja ni kuongeza misaada na kubadilisha sera ya uhamiaji ili kuharakisha zoezi la kuwarudisha wahamiaji wanaoingia kinyume cha sheria barani ulaya.

Akizungumzia suala hilo, Rais wa Kamisheni ya Ulaya, Ursula von der Leyen, amesema..

"Leo tunaona kwamba katika wale wote ambao hawana haki ya kukaa katika Umoja wa Ulaya, ni 20% tu ya wale ambao wana uamuzi wa kurejea ndio wanarudishwa katika nchi zao za asili. Kwa hiyo tunafanya kazi ili kuboresha uendeshaji na sisi hivi karibuni tutawasilisha pendekezo jipya. Pendekezo la kisheria tulilokuwa nalo toka 2018 limekwama katika Bunge na Baraza. Kwa hivyo tutakuja na pendekezo jipya kwa mara nyingine.", alisema Von der Leyen.

Uhamiaji ni mada nyeti katika nchi zote 27 wanachama wa Umoja huo. Wahamiaji 250,000 waliingia Ulaya mwaka uliopita ingawa mwaka huu idadi yao imepungua.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW