SiasaBelarus
EU yakubali kuchukua hatua za vikwazo vikali kwa Belarus
26 Julai 2023Matangazo
Uhispania ambayo ni rais wa kupokezana wa Umoja wa Ulaya imetoa tamko hilo leo hii Jumatano. Mabalozi wa nchi za Umoja wa Ulaya wamekubaliana kwa kauli moja juu ya hatua hizo kali kwa kuzingatia hali ya Belarus na ushiriki wa nchi hiyo katika uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.
Hatua hizo ni pamoja na kuwaweka kwenye orodha ya vikwazo watu binafsi na taasisi umesema Umoja wa Ulaya katika tamko lake lililochapishwa mtandaoni.