1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Umoja wa Ulaya walaani machafuko Mashariki ya Kati

8 Aprili 2023

Umoja wa Ulaya umelaani mashambulizi yaliyosababisha vifo nchini Israel pamoja na makombora yaliyofyetuliwa kutokea Lebanon ambayo lsrael ilijibu kwa kufanya hujuma za kijeshi ikiwemo dhidi ya ukanda wa Gaza.

Uharibifu baada ya shambulizi la ndege za Israel
Mashambulizi ya Israel kujibu makombora yaliyofyetuliwa na wanamgambo wa Kipalestina yameacha uharibifu wa majengo nchini LebanonPicha: Mahmoud Zayyat/AFP/Getty Images

Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borell amesema Ulaya inakosoa vikali matendo hayo ya kikatili na kuzitaka pande zote kusitisha maramoja makabiliano pamoja na kujizuia kutanua uhasama.

Wasiwasi wa kuzuka mapigano eneo la Mashariki ya Kati unaongezeka tangu kutokea shambulizi la bunduki lilowaua raia wawili wenye nasaba ya Israel huko Ukingo wa Magharibi na shambulizi jingine kumuua mtaalii wa kitaliana mjini Tel Aviv.

Matukio hayo yamejiri baada ya polisi ya Israel kupambana na Wapalestina mnamo siku ya Jumatano ndani ya msikiti wa Al-Aqsa mjini Jerusalem.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW