Umoja wa Ulaya walaani shambulio la al-Shabaab
25 Agosti 2010Matangazo
Katika shambulio hilo,wanamgambo wa kundi la al-Shabaab waliovaa sare ya jeshi la serikali,walivamia hoteli moja na walipambana na vikosi vya usalama kwa saa nzima kabla ya kuripua mabomu.
Ashton amesema, Umoja wa Ulaya unashikamana na umma wa Somalia na utaendelea kuisaidia serikali ya mpito ya nchi hiyo.
Hata Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na maafisa wa serikali ya Marekani wamelaani vikali shambulio la wanamgambo hao wa Kisomali. Shambulio hilo limetokea siku ya pili ya mapigano makali yaliyozuka mjini Mogadishu ambayo hadi sasa yamesababisha vifo vya watu 70.
Mwandishi: P.Martin/ZPR