SiasaUkraine
Umoja wa Ulaya wapendekeza vikwazo vipya dhidi ya Urusi
8 Mei 2023Matangazo
Msemaji wa halmashauri hiyo, Eric Mamer amesema vikwazo vipya vitajikita katika kuimarisha ufanisi wa vikwazo vya awali na kuzuia ukwepaji wa vikwazo hivyo.
Mojawapo ya mapendekezo hayo ni kusimamisha mauazo ya teknolojia ya hali ya juu kwa makampuni manane ya Kichina, ambayo yanashukiwa kuiuza tena kwa Urusi.
Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi 27 wanachama wa Umoja wa Ulaya watakutana mjini Brussels Jumatano wiki hii kujadili mapendekezo hayo ya halmashauri kuu.
Baadhi ya wanadiplomasia wa Ulaya wanakiri kuwa umoja huo unakaribia mwisho wa aina ya vikwazo wanavyoweza kuafikiana kuiwekea Urusi, baada ya kupitisha awamu 10 ya vikwazo vya pamoja.