1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Ulaya wapongeza matokeo ya uchaguzi nchini Moldova

29 Septemba 2025

Umoja wa Ulaya umepongeza matokeo ya uchaguzi wa bunge nchini Moldova na kusema umeonyesha kuwa nchi hiyo ndogo ya mashariki mwa Ulaya iko kwenye njia sahihi ya kujiunga na Umoja huo.

 Berlin 2025 | Ursula von der Leyen
Rais wa halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya, Ursula von der LeyenPicha: Bernd von Jutrczenka/dpa/picture alliance

Kwenye chapisho kwenye mtandao wa X, Rais wa Baraza la Ulaya Antonio Costa, amesema watu wa nchi hiyo wametuma ujumbe ulio wazi.

Costa amesema wamechagua demokrasia, mageuzi, na mustakabali wa Ulaya, chini ya muingilio na shinikizo la Urusi.

Kwa upande wake, Rais wa halmashauri kuu ya Umoja huo wa Ulaya Ursula von der Leyen, amesema ni wazi Moldova imepigia kura Ulaya, demokrasia na uhuru .

Ameongeza kusema, mlango wa Umoja huo uko wazi na watasimama na nchi hiyo katika kila hatua.

Moldova yathibitisha kujinasua kutoka mzunguko wa Urusi

Ushindi huo mkubwa dhidi ya upinzani unaoegemea upande wa Urusi, unaonyesha uidhinishaji wa nchi hiyo iliyokuwa jamhuri ya Kisovieti ya kutaka kujiunga na Umoja wa Ulaya na kujinasua kutoka kwa mzunguko wa Urusi.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW