1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Ulaya washinikizwa kukatiza msaada kwa Rwanda

14 Februari 2025

Bunge la Ulaya limeutaka Umoja wa Ulaya kusitisha kuiunga mkono moja kwa moja bajeti ya umoja huo kwa Rwanda hadi nchi hiyo itakapovunja uhusiano wake na waasi wa kundi la M23.

Mkuu wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya Joseph Borrell akitoa hotuba wakati wa mjadala kuhusu kuongezeka kwa mgogoro katika Mashariki ya Kati na hali nchini Lebanon huko Strasbourg mnamo Oktoba 8.2024
Kikao cha bunge la Umoja wa Ulaya Picha: FREDERICK FLORIN/AFP

Bunge la Ulaya pia limetoa wito wa kusitishwa kwa mkataba wa maelewano kati ya Rwanda na Umoja wa Ulaya ambao unalenga kusaidia usambazaji wa madini ya kimkakati ya Rwanda hadi wakati ambapo nchi hiyo itaacha kuiingilia Kongo.

Uvamizi wa Kongo ni ukiukaji usiokubalika wa uhuru wa nchi hiyo

Bunge la Ulaya limesema linalaani vikali uvamizi wa Goma na maeneo mengine ya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo unaofanywa na waasi wa M23 waasi na vikosi vya ulinzi vya Rwanda na kuutaja kuwa ukiukaji usiokubalika wa uhuru na uadilifu wa Kongo.

Azimio la kusitisha msaada kwa Rwanda laungwa mkono 

Bunge lilipitisha azimio hilo, hizi zikiwa juhudi za shinikizo la kisiasa kwa halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya na mataifa wanachama wa Umoja huo katika kura iliyoungwa mkono na wabunge 443 dhidi ya 4 waliopinga huku wengine 48 wakikosa kushiriki katika kura hiyo.

Waasi wanaoungwa mkono na Rwanda wadai kuuteka mji wa Goma

Katika maoni kwa jopo la bunge hilo la Ulaya jana, balozi wa Rwanda nchini Ujerumani, Igor Cesar, alisema kuwa nchi yake sio chanzo cha mgogoro huo wala haina jukumu la kuutatua peke yake.

Rais wa Rwanda, Paul KagamePicha: Utku Ucrak/Anadolu/picture alliance

Msemaji wa serikali ya Rwanda Yolande Makolo hakujibu kwa haraka ombi la tamko kuhusu suala hilo.

Tshisekedi kushiriki katika mkutano wa kilele wa Umoja wa Afrika 

Rais wa Kongo Félix Tshisekedi, atashiriki katika mkutano wa kilele wa Umoja wa Afrika wikendi hii nchini Ethiopia hapo kesho, lakini hatahudhuria mkutano kuhusu mgogoro wa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Kitengo cha mawasiliano cha ofisi ya rais kimeliarifu shirika la habari la AFP hapo jana.

Kitengo hicho kimeongeza kuwa ni waziri mkuu Judith Suminwa Tuluka) atakayehudhuria mkutano huo wa Baraza la Amani na Usalama.

Mkutano rasmi wa kilele wa Umoja huo wa Afrika unatarajiwa kufanyika siku ya Jumamosi na Jumapili na utajumuisha uchaguzi wa mwenyekiti mpya wa Halmashauri ya Umoja wa Afrika.

Waasi wa M23 waudhibiti mji wa kimkakati wa mashariki ya Kongo

Katika taarifa iliyotolewa jana jioni, ofisi hiyo imesema kuwa Tshisekedi amewasili nchini Ujerumani kushiriki Mkutano wa Usalama wa Munich unaoanza leo hadi siku ya Jumapili.

UNICEF yaonya kuhusu ubakaji na ukatili dhidi ya watoto Kongo

Mkurugenzi mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia watoto UNICEF Catherine Russell, ameonya jana kuwa ubakaji na ukatili mwingine dhidi ya watoto mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo umeongezeka kwa viwango vya juu mno.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW