Umoja wa Ulaya washutumu mashambulio nchini Iraq
23 Desemba 2011Matangazo
Mkuu wa sera za mambo ya kigeni wa Umoja wa Ulaya Catherine Ashton ameshutumu vikali mashambulio ya jana Alhamis mjini Baghdad ambapo watu 67 wameuwawa na amewataka viongozi wa Iraq kuanzisha majadiliano mara moja ili kutatua tofauti zao. Katika taarifa Ashton ameshutumu upotevu wa maisha uliosababishwa na magaidi wanaotumia hali tete iliyopo ya kisiasa. Miripuko ilitokea katika maeneo 14 tofauti, ililenga maeneo ya Washia. Polisi ya Iraq inatuhumu wanamgambo wa Kisunni kuwa wanahusika na mashambulio hayo. Waziri mkuu wa Iraq Nuri al-Maliki ameahidi kuwa washambuliaji hatawaruhusiwa kuleta athari yoyote katika hatua za kisiasa, wakati spika wa bunge Osama al-Nujaifi ameshutumu mashambulio hayo, ambayo amesema yanatishia umoja wa kitaifa.