Umoja wa Ulaya wasikitishwa na mauaji ya raia 1,000 Darfur
13 Novemba 2023Umoja wa Ulaya umeelezea kushtushwa na ripoti za mauaji ya watu zaidi ya 1,000 katika eneo la Darfur Magharibi mwa Sudan. Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell alisema jana kwamba mauaji hayo ya hivi karibuni yanaonekana kuwa sehemu ya kampeni pana ya safisha ya kikabila iliyoendeshwa na wanamgambo wa kundi la RSF kwa lengo la kutokomeza jamii ya Masalit ambayo sio Waarabu kutoka Darfur Magharibi.UN: Nusu ya raia wa Sudan wanahitaji msaada wa kiutu
Taarifa ya Umoja wa Ulaya inasema inazo ripoti za mashahidi wa kuaminika za mauaji hayo huko Ardamta, magharibi mwa mkoa wa Darfur ndani ya siku mbili. Umoja huo umeonya juu ya hatari ya mauaji mengine ya halaiki mkoani Darfur.
Idadi hiyo ni kubwa kuliko iliyotolewa awali na shirika la wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR ya watu 800.