1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

EU yataka bajeti ya jeshi la Urusi idhibitiwe

26 Novemba 2025

Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya, Kaja Kallas amesema bajeti ya jeshi la Urusi inapaswa kudhibitiwa ili kuhakikisha mzozo unaoendelea nchini Ukraine unamalizika.

Kaja Kallas
Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Kaja KallasPicha: Alexandros Michailidis/European Union

Kallas ameyasema hayo mbele ya waandishi wa habari mjini Brussels na kuongeza kuwa makubaliano yoyote ya amani yanahitaji kuihusisha pia Urusi.

Naye Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz akihutubia mbele ya bunge mjini Berlin kuhusu mzozo huo huo ameeleza kwamba makubaliano ya amani ya Ukraine hayawezi kutiwa saini bila idhini ya Ukraine na Ulaya.

Uamuzi kuhusu Ulaya utafanywa na Ulaya

Amesema juhudi za Marekani kuutatua mzozo huo zinakaribishwa, lakini uamuzi kuhusu masuala ya Ulaya yanaweza kufanywa kwa makubaliano na Ulaya pekee.

Kauli za Kallas na Merz zimetolewa wakati Marekani ikitarajiwa kufanya majadiliano na Urusi hivi karibuni kuhusu mpango wa kuvimaliza vita vya Ukraine wenye vipengele 28 uliowasilishwa na Rais Donald Trump.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW