1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Ulaya wataka Bazoum aachiliwe huru

27 Julai 2023

Umoja wa Ulaya leo umetoa wito wa "kuachiwa mara moja" kwa Rais wa Niger Mohamed Bazoum na familia yake, baada ya maafisa wake wa ulinzi kumshikilia na kudai kwamba wamechukua madaraka.

Ägypten Niger Präsident  Mohamed Bazoum
Picha: Ludovic Marin/AFP

Msemaji wa Umoja wa Ulaya, Nabila Massrali, amesema Niger ni mshirika muhimu wa Umoja huo katika kanda ya Sahel na kutikiswa kwake hakutokuwa na manufaa ya kitaifa, kikanda na hata zaidi kwa yeyote yule.

Haya yanajiri wakati ambapo jeshi la Niger, limewaunga mkono rasmi viongozi wa mapinduzi na hatua yao ya kutaka kuufikisha mwisho muhula wa Bazoum.

Soma zaidi: Jeshi na wananchi waunga mkono mapinduzi ya Niger

Taarifa hiyo ya jeshi imechapishwa katika kurasa za mitandao ya kijamii ya Facebook na Twitter.

Hatua hiyo ya jeshi kuwaunga mkono viongozi hao wa mapinduzi inatarajiwa kummaliza kisiasa Rais Mohamed Bazoum.